Albamu ya msanii wa Bongo Fleva nchini Tanzania Ibraah aliyoipa jina la “1B : The Other Side of the Face” itakuwa na nyimbo 50!
Msanii huyo ameelezea kuwa kazi hiyo ya sanaa, itakuwa na ladha tofauti za muziki na simulizi mbalimbali za maisha.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ibraah amesema albamu hiyo itakuwa na nyimbo zinazozungumzia mapenzi, maumivu ya kuachwa, maisha ya kila siku, pamoja na nyimbo za burudani na mitaani.
Aidha, Ibraah amefichua kuwa albamu hiyo itahusisha ushirikiano na Wasanii mbalimbali, wakiwemo Phina, Chid Benz, King Kaka, Dully Sykes na Paato, pamoja na Wasanii wengine watano.
Ibraah amesema albamu hiyo si mkusanyiko wa nyimbo pekee, bali ni uzoefu wa kipekee wa kimuziki, huku akiwataka Mashabiki wake kuchagua nyimbo tatu zinazowavutia zaidi katika orodha aliyotangaza.
Jina halisi la msanii huyo ni Ibrahim Abdallah Nampunga na ingawa alipenda muziki kuanzia utotoni, alijipatia umaarufu Aprili 2020, alipotangazwa msanii wa kwanza kusajiliwa na kampuni ya Harmonize ya Konde Worldwide Music.
Akiwa chini ya usimamizi wa Konde Music, alitoa mkusanyiko wa nyimbo alioupa jina la “Steps”.
Baadaye aligura Konde Music akawa msanii huru na kuendelea na kazi za muziki akitoa nyimbo kama “One Night Stand” na “Dharau.