Timu ya Kenya ya wanawake walio chini ya umri wa miaka 17-Junior Starlets, inaendelea na mazoezi yake nchini Morocco, kujiandaa kwa fainali za Kombe la Dunia kuanzia Jumamosi hii.
Starlets inayonolewa na Midred Cheche itafungua kampeni ya kushiriki Kombe la Dunia kwa mara ya pili kundini E,dhidi ya Uchina Oktoba 19 ,kabla ya kukabiliana na Marekani tarehe 22 na hatimaye dhidi ya Samoa siku tatu baadaye.
Kombe la Dunia kwa wanawake chini ya umri wa miaka 17,litaanza Jumamosi hii Ujerumani wakikabiliana na Argentina kundini A kabla ya wenyeji Morocco kumaliza udhia na New Zealand.