Mauaji ya mwanasheria Mbobu: DPP aidhinisha mashtaka dhidi ya washukiwa 5

Mbobu, ambaye alikuwa mhadhiri na mwandishi, alifyatuliwa risasi na kuuawa Septemba 9 mwaka jana wakati akirejea nyumbani kwake mtaani Karen jijini Nairobi.

Martin Mwanje
1 Min Read
Rose Mbithe (katikati) na wanawe

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, DPP ameidhinisha mashtaka ya mauaji dhidi ya washukiwa watano katika kesi ya mauaji ya mwanasheria Mathew Kyalo Mbolu yaliyotokea mwaka jana.

Watano hao ni pamoja na mwanasiasa Rose Mbithe Mulwa, wanawe wawili Chris Mulwa na Angela Mulwa, na makonstebo wawili wa polisi, Julius Kipkoech Cheruiyot na Kennedy Kipkemei Borboroi.

Cheruiyot na Borboroi walifikishwa mbele ya Jaji Diana Kavedza wa Mahakama Kuu ya Kibera lakini hawakujibu mashtaka.

Mahakama iliagiza kuwa wafanyiwe uchunguzi wa akili katika hospitali ya Mbagathi.

Jaji Kavedza pia aliagiza Bi. Mbithe na Bi. Mulwa, ambao wanazuiliwa katika gereza la wanawake la Lang’ata na Bw. Mulwa, anayezuiliwa katika gereza la Nairobi Remand and Allocation kufikishwa mahakamani.

Watatu hao pia wanakabiliwa na kesi nyingine ya mauaji ya Dkt. Victoria Mutiso.

Washukiwa hao watano wamepangiwa kusomewa mashtaka Oktoba 27 mwaka huu baada ya mahakama kupokea ripoti ya uchunguzi wa akili.

Mwanasheria Mbobu, ambaye alikuwa mhadhiri na mwandishi, alifyatuliwa risasi na kuuawa Septemba 9 mwaka jana wakati akirejea nyumbani kwake mtaani Karen jijini Nairobi.

Share This Article