Serikali kutoongeza kandarasi za hospitali za SHA baada ya Oktoba 14

Kulingana na mpangilio huo hospitali na vituo vya afya aidha vya viwango vya Level 4 au Level 5 zitatoa tu huduma zilizodhishwa kutoa.

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali kamwe haitongeza muda wa kandarasi zilizopo katika bima ya afya ya umma SHA punde muda wake mikataba ya sasa utakapokamilika tarehe 14 mwezi huu.

Haya yameafikiwa Jumatatu kati ya waziri wa Afya Aden Duale na kamati ya Afya katika baraza la Magavana nchini CoG .

Katika kikao hicho kilichoongozwa na mwenyekiti wa kamati ya afya katika  COG ambaye pia ni Gavana wa Mombasa Abdulswamad Nassir  na Duale aidha, kiliafikia kuanza mchakato wa kusaini kandarasi mpya za hospitali zitakazotoa huduma za matibabu baina ya mwaka 2026 na 2029.

Hata hivyo, serikali imetoa hakikisho la kukamilisha utoaji kandarasi kwa wakati ufaao ili kuhakikisha wagonjwa wanapokea huduma za matibabu bila tatizo lolote.

Kikao hicho kimeshirikisha pia maafisa wa SHA,Shirika la Digital Health Agency (DHA) na wasiamamizi wa utoaji huduma za matibabu,  ili kutekeleza mikataba mipya ya miaka mitatu ijayo.

Kulingana na mpangilio huo hospitali na vituo vya afya aidha vya viwango vya Level 4 au Level 5 zitatoa tu huduma zilizodhishwa kutoa.

Share This Article