Ni rasmi Seneta Sifuna kuwania urais kwa chama cha TEP

Kiongozi wa TEP Gilbert Marava, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya Jumapili, alisema walilazimika kubadilisha mfumo wa uongozi wa chama ili kubuni nafasi kwa Sifuna na wafuasi wake.

Dismas Otuke
1 Min Read

Seneta wa Nairobi ambaye pia ni kiongozi wa vuguvugu la Linda Mwananchi Edwin Sifuna, ametangaza kuwania kiti cha urais mwaka ujao kwa tiketi ya The Equitable Party (TEP).

Uzinduzi wa chama hicho ulifanyika jana Jumapili katika kaunti ya Nairobi na kuhudhuria na viongozi wengi wa upinzani.

Kiongozi wa TEP Gilbert Marava, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya Jumapili, alisema walilazimika kubadilisha mfumo wa uongozi wa chama ili kubuni nafasi kwa Sifuna na wafuasi wake.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Magavana George Natembeya wa Trans Nzoia, James Orengo wa Siaya, Rais wa zamani wa Chama cha Mawakili nchini (LSK) Faith Odhiambo, wabunge Babu Owino wa Embakasi East, Anthony Kibagendi wa Kitutu Chache South, Majimbo Kalasinga kutoka Kabuchai, Jack Wamboka wa Bumula, Patrick Simiyu wa Cheragany, Patrick Makau kutoka Mavoko, na Clive Ombane Gisairo wa Kitutu Masaba.

Share This Article