Rais wa WADA Witold Bańka awasili Kenya kwa ziara ya siku tatu

Bańka anatarajiwa kutathmini maendeleo yaliyopigwa na Kenya kupitia kwa shirika kupambana na ulaji muku nchini (ADAK).

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Shirikisho la kukabiliana na matumizi ya dawa ya kuongeza mwilini (WADA) Witold Bańka, yuko nchini Kenya kwa ziara rasmi ya siku tatu.

Witold Bańka alitua katika angatua ya kimataifa ya JKIA mapema Jumapuli na atarajiwa kukutoka na Rais William Ruto katika Ikulu ya Nairobi kando na kukutana na viongozi wa kamati ya Olimpiki nchini NOCK siku ya Jumanne kabla ya kuwahutubia Wanahabari.

Bańka anatarajiwa kutathmini maendeleo yaliyopigwa na Kenya kupitia kwa shirika kupambana na ulaji muku nchini (ADAK).

Aidha kiongozi huyo anatarajiwa kufanya kikao na wanamichezo na maafisa wakuu serikalini.

Share This Article