Shujaa yaibwaga Madagascar,yatwaa taji ya Mauritius Sevens

Awali Shujaa ilikuwa imeicharaza Afrika Kusini pointi 15-0, katika nusu fainali.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wanaume saba upande almaarufu Shujaa, imeilemea Madagascar pointi 15-12 ,na kunyakua taji ya Mauritius Seven’s kwenye fainali ya Jumapili.

Awali Shujaa ilikuwa imeicharaza Afrika Kusini pointi 15-0, katika nusu fainali.

Afrika Kusini ilinyakua nishani ya shaba kufuatia ushindi wa alama 22-14, dhidi ya Burkina Fasso.

Aidha,Afrika Kusini ilishinda taji ya wanawake kwa ushindi wa alama 22-10, dhidi ya wenyeji Mauritius.

Share This Article