Mathew Sawe atajitosa uwanjani Jumapili kutetea taji la mbio za London Marathon nchini Uingereza kwa wanaume.
Sawe atakabiliana na upinzani mkali kutoka kwa Waganda Joshua Cheptegei na Jacob Kiplimo na wanariadha kutoka Ethiopia Tamirat Tola na Yomif Kejelcha.
Mbio za wanawake zitawashirikisha Wakenya Hellen Obiri na Joyceline Jepkosgei watakaopambana na bingwa mtetezi Tigst Assefa .
Mbio za London zitakuwa za tatu katika msururu wa mbio kuu ulimwenguni baada ya Tokyo Marathon mwezi jana na Boston Marathon Jumatatu wiki hii.