Murkomen: Serikali imepiga hatua kurejesha usalama Kerio Valley

Murkomen alisema operesheni za kijasusi zinazolenga kutwaa silaha zinaendelea pamoja na mashauriano na jamii kulinda maeneo yaliyosalia.

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen, ashiriki mazungumzo na viongozi wa Pokot Magharibi.

Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen, amesema serikali imepiga hatua kurejesha usalama na amani katika eneo la Bonde la Kerio, kaunti ya Pokot Magharibi.

Akizungumza aliposhiriki mazungumzo na viongozi kutoka Pokot Magharibi. Murkomen alisema operesheni za kijasusi zinazolenga kutwaa silaha zinaendelea pamoja na mashauriano na jamii kulinda maeneo yaliyosalia.

“Tulikubaliana kuwapa mafunzo na kuwapeleka maafisa zaidi wa polisi wa akiba kwenye maeneo yanayokumbwa na changamoto za kiusalama, kufungua vituo vya kiutawala, kupeleka magari zaidi, kuwiainisha miundombinu ya kusalama ili kuafikia mahitaji ya kiusalama na kuwahamisha maafisa maafisa ambao wamekaa kwa muda mrefu,” alisema Murkomen.

Wakati huo huo, Murkomen alisema atashiriki meza ya mazungumzo na viongozi kutoka kaunti ya Turkana pamoja na Wizara ya Madini, ili kuimarisha usalama katika maeneo ya uchimbaji madini.

Aidha,  alitangaza kuharakishwa kwa utoaji wa vitambulisho vya kitaifa  katika jamii ambazo hazijafikiwa na huduma hizo.

Share This Article