Serikali yaidhinisha shilingi bilioni 6.4 kwa upanuzi wa NYS

Waziri wa Utumishi wa Umma Geoffrey Ruku, amesema uwekezaji huo utafadhili madarasa zaidi, karakana, kambi, na vifaa vya usimamizi katika taasisi zote za NYS nchini.

Tom Mathinji
1 Min Read
Serikali yaidhinisha shilingi bilioni 6.4 kwa upanuzi wa NYS
Serikali imeidhinisha shilingi bilioni 6.4 kwa upanuzi wa miundombinu katika Huduma ya Taifa kwa Vijana (NYS), ili iweze kumudu idadi inayoongezeka ya makurutu.

Waziri wa Utumishi wa Umma Geoffrey Ruku, amesema uwekezaji huo utafadhili madarasa zaidi, karakana, kambi, na vifaa vya usimamizi katika taasisi zote za NYS nchini.

Ruku, aliyemwakilisha Rais William Ruto kwenye sherehe ya kufuzu kwa makurutu wa NYS  katika kambi ya Gilgil, kaunti ya Nakuru, alidokeza kuwa upanuzi wa miundombinu utafanikisha huduma hiyo kuwahifadhi makurutu 50,000 kila wakati.

“Hapo awali Rais aliagiza kuongezwa kwa makurutu wa NYS hadi 100,000 kufikia mwaka 2028. Idadi hiyo inapaswa kuambatana na upanuzi wa miundombinu, vifaa, pamoja na uwezo wa kuwahudumia wafanyakazi,” alisema Ruku.

Aidha, waziri huyo alidokeza kuwa mafunzo ya kiufundi pia utapanuliwa kuhakikisha makurutu wanafuzu wakiwa na ujuzi ulio na ushindani mkubwa kwenye soko la ajira.

Share This Article