Rais William Ruto ametuma risala za rambirambi kwa familia na watu wa Zimbabwe kufuatia kifo cha ghafla cha mfanyabiashara Wicknell Chivayo.
Chivayo alifariki jana Jumatano jioni viungani mwa mji wa Harare kwenye ajali ya ndege aina ya helikopta pamoja na mkewe Lucy Muteke na watu wengine wanne.
Ruto amemtaja marehemu kuwa raifiki wa karibu aliyekuwa na maono makubwa kuhusu uwezo wa bara la Afrika, akisema kifo hicho ni cha kusikitisha.
Rais Ruto ametuma risala za rambirambi kwa Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa na familia za watu wote sita walioangamia kwenye ajali hiyo.
Chivayo amewahi kukutana na Rais Ruto katika Ikulu ya Nairobi awali, na madai ya mfanyabiashara huyo kupewa kandarasi ya kukarabati Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, JKIA yalipuuziliwa mbali na serikali.