Bwanyenye wa Zimbabwe Wicknell Chivayo na mkewe Lucy Muteke ni miongoni mwa watu sita ambao wamethibitishwa kufariki katika ajali ya ndege Jumatano jioni katika mji mkuu wa nchi hiyo, Harare.
Kulingana na msemaji mkuu wa serikali Nick Mangwana, ajali hiyo ilitokea mashariki mwa mji huo baada ya helikopta iliyokuwa imewabeba kuanguka na kuua abiria wote sita.
Chanzo cha ajali hiyo iliyotokea katika kijiji cha Marondera bado hakijajulikana.
Chivayo alikuwa mwandani wa viongozi wengi barani Afrika, akiwemo Rais William Ruto.
Bwanyenye huyo aliye na umri wa miaka 43, hufanya biashara nyingi nchini zimbabwe zikiwemo za sekta ya mafuta, zabuni na miundombinu.