Harambee Stars kumenyana na Guinea mjini Conakry

Timu zote zinatoshana nguvu katika rekodi ya mechi za awali kila moja ikishinda mechi of 4, kuelekea kwa mechi ya tisa leo.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars itakuwa na kibarua kigumu itakaposhuka mjini Conakry leo Alhamisi jioni kwa mechi ya pili ya kundi D, kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka ujao.

Kenya iliyo na alama moja pekee baada ya kutoka sare na Eritrea katika mechi ya kwanza wiki jana, itajizatiti kusajili matokeo mazuri kama sehemu ya maandalizi kwa kipute cha AFCON ambacho itaandaa kwa pamoja na Tanzania na Uganda.

Afrika Kusini wanaongoza kundi hilo kwa alama sita baada ya kusajili ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Eritrea.

Guinea kwa upande wao watakuwa wakisaka ushindi wa kwanza baada ya kushindwa na Afrika Kusini mabao 2-1 katika mechi ya ufunguzi.

Vijana wa Benny McCarthy walifanyza mazoezi ya mwisho jana jioni kujiandaa kwa mechi ya leo.

Mchuano huo utang’oa nanga saa moja usiku katika uchanjaa wa September 28, mjini Conakry .

Guinea, almaarufu Syli Nationale, wanashikilia nafasi ya 81 katika msimamo wa FIFA huku Kenya ikiwa ya 109.

c

Share This Article