Mfalme Mohammed wa sita amteua Fatima Ezzahra kuwa Waziri Mkuu wa Morocco

Dismas Otuke
1 Min Read

Mfalme Mohammed wa sita amemteua Fatima Ezzahra kuwa Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke nchini Morocco. 

Uteuzi huo ulifanywa kwa mujibu kwa ibara ya 47 ya katiba ya nchi hiyo.

Nao ulitangazwa kufuatia mkutano ulioandaliwa kwenye Kasri ya Rabat na kuongozwa na Mfalme.

Ezzahra ambaye hadi uteuzi wake alikuwa mshirikishi wa shughuli za chama cha Authenticity and Modernity, kilichotwaa viti vingi katika uchaguzi wa mwezi jana, amekuwa mwanamke wa kwanza kupewa wadhifa huo mkuu serikalini.

Katika hotuba yake ya kwanza,  Waziri Mkuu huyo mpya alitaja uteuzi wake kuwa wa kihistoria akiahidi serikali itakayotimiza ndoto za raia wa Morocco na maono ya Mfalme Mohammed wa sita.

Share This Article