Waziri wa Michezo Salim Mvurya amempokea Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kandanda Afrika (CAF) Samson Adamu, aliyewasili nchini Kenya siku ya Jumatatu kukagua maandalizi ya makala ya 36 ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka ujao.
Adamu, aliyepokelewa na Katibu wa Wizara ya Michezo Elijah Mwangi, alizuru viwanja vya Kasarani na Raila Odinga kubaini matayarisho yake kwa kuandaa mechi za AFCON.
Kenya inatarajiwa kuandaa kipute cha AFCON kwa pamoja na mataifa jirani ya Uganda na Tanzania kati ya Juni 19 na Julai 17 mwaka ujao.
Adamu, ambaye ni raia wa Nigeria, anazuru Kenya takriban miezi miwili kabla ya kufunguliwa rasmi kwa uga wa Raila Odinga, unaotarajiwa kufunguliwa Januari tano mwakani kwa mechi ya kirafiki baina ya miamba wa Ulaya Bayern Munich ya Ujerumani na Ajax Amsterderm kutoka Uholanzi.