Afueni! Washinde wa uchaguzi mkuu mwakani kuteuliwa bungeni

Dismas Otuke
1 Min Read
Vikao vya bunge la taifa.

Ni afueni kwa wagombea wa uchaguzi mkuu katika viti vya urais na naibu wake watakaoshindwa debeni kwani sasa wanaweza kuteuliwa na chama chao husika kuwa wabunge.

Hii ni baada ya bunge la kitaifa kufanyia marekebisho sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC)  ya mwaka 2024, ibara ya 9, ambapo sasa wataingia bungeni kupitia uteuzi wa vyama vyao.

Awali, sheria ya uchaguzi iliwafungia nje wapeperushaji bendera ya urais na manaibu wao kutoka vyama vya kisiasa kuteuliwa bungeni.

Hatua hiyo ilifuatia agizo la mahakama lililosema kuwa kuwafungia nje wagombea hao katika uteuzi wa bunge ni kinyume cha katiba na ukiukaji wa sheria.

Share This Article