Kenya yaipongeza Ureno kwa kufungua kituo cha visa Nairobi

Rais Ruto alikariri kujitolea kwa Kenya kuendelea kushirikiana kwa karibu na Rais mpya wa Ureno António José Seguro.

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William ashiriki mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Portugal Paulo Rangel.

Rais William Ruto amesema Kenya na Ureno zinadhamini kwa dhati ushirikiano wa muda mrefu, ulioanzishwa miongo mitano iliyopita.

Akizungumza aliposhiriki mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ureno Paulo Rangel katika ikulu ya Nairobi, kiongozi wa Taifa alisema nchi hizo mbili zimejitolea kuboresha biashara na kupanua soko kwa bidhaa za Kenya hususan bidhaa zilizoongezwa thamani za kilimo.

“Zaidi ya biashara, tunabuni njia za kupanua uwekezaji, ushirikiano wa shughuli za majini na uhamiaji, kuambatana na kujitolea kwetu kuhakikisha raia wetu wanafaidika,’ alisema Rais Ruto.

Rais Ruto alipongeza Ureno kwa kufungua kituo cha Visa Jijini Nairobi, kufanikisha shughuli za wakenya wanaosafiri kuelekea Ureno.

Aidha, Rais alikariri kujitolea kwa Kenya kuendelea kushirikiana kwa karibu na Rais mpya wa Ureno António José Seguro.

Share This Article