Rais William Ruto anatarajiwa kumpokea mshikilizi mpya wa rekodi ya dunia ya mbio za Marathon, Sabastian Sawe leo.
Hafla hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na vingozi kutoka wizara ya michezo akiwemo Waziri Salim Mvurya, na wale wa chama cha Riadha Kenya.

Sawe aliye na umri wa miaka 31, aliweka rekodi mpya ya dunia saa 1 dakika 59 na sekunde 30 ,alipotwaa ushindi katika mbio za London Marathon.

Mwanariadha huyo alirejea nchini Jumatano usiku akitumia ndege ya Kenya Airways, na kupokelewa na idadi kubwa ya watu katika uwanja wa JKIA.

Sawe ambaye ni mzawa wa kaunti ya Nandi, ndiye mwanariadha wa kwanza kukamilisha marathon kwa chini ya saa 2,akivunja rekodi ya marehemu Kelvin Kiptum yam waka 2023 ya saa 2 na sekunde 35.
Ruto anatarajiwa kumtuza Sawe shilingi milioni 5, zilizopitishwa na bunge kuwa tuzo kwa mwanariadha anayevunja rekodi ya dunia.