Dudubaya kuhusishwa 30 ya Bongo Fleva kwa mkataba

Hii ni baada ya msanii huyo kukiuka masharti ya maadili na kusababisha yeye na mratibu wa tamasha hiyo kutozwa faini na BASATA.

Marion Bosire
1 Min Read

Msanii mkongwe wa muziki nchini Tanzania Godfrey Tumaini, maarufu kama Dudubaya, sasa atakuwa akihusishwa kwenye tamasha za miaka 30 ya Bongo Fleva kwa njia ya mkataba.

Hii ni baada ya msanii huyo kukiuka masharti ya maadili na kusababisha yeye na mratibu mkuu wa tamasha hiyo ya miaka 30 ya Bongo Fleva, kutozwa faini na Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA.

Mratibu mkuu wa tamasha hiyo ambaye pia ni msanii Madee Ally, amesema hakuwa anafahamu kabisa aina ya wasanii anaohusiana nao katika kazi yake, kutokana na miaka mingi bila wakongwe wa muziki kupanda jukwaani.

Sasa Ally amesema kuna sheria mpya za wasanii tofauti na kipindi cha nyuma alitegemea kukumbana na changamoto za ukiukwaji wa sheria kwa msanii au kundi la muziki.

Aidha katika mwendelezo wa tamasha hiyo, Ally amesema kila msanii atawajibika mwenyewe kutokana na mkataba atakaoingia na waandalizi.

“Endapo utakiuka haya masharti ambayo tumekuwekea (lugha isiyo na staha, matusi, kupigana) basi utakuwa nje ya makubaliano,” alisema Madee akiongeza kwamba hiyo ndiyo njia watatagusana na Dudubaya.

Tayari Madee amelipa faini ya shilingi milioni 3 pesa za Tanzania yake binafsi pamoja na nyingine sawia ya Dudubaya. Awamu ijayo ya tamasha hiyo ni ya Zanzibar, Oktoba 17, 2026.

Share This Article