Viongozi watakiwa kuwekeza katika miradi ya kuwawezesha vijana

KBC Digital News
1 Min Read

Washikadau na viongozi wametakiwa kuwekeza zaidi katika miradi itakayowawezesha vijana kujiendeleza kiufundi.

Mwakilishi wa Wanawake katika kaunti ya Machakos, Kamene Kasimbi, amesema vijana wataweza kupunguza pengo la ajira ikiwa watapatiwa ujuzi wa kiufundi.

Akizungumza katika hafla ya mahafali ya vijana aliowafadhili masomo ya kiufundi, Kasimbi amewataka viongozi kuwekeza kwa vijana badala ya miradi isiyobuni ajira.

Kauli yake iliungwa mkono na Mkurugenzi wa Chuo cha Kiufundi cha Great Nairobi East College, Mary Kimanzi, aliyehimiza vijana kupata ujuzi wa kiufundi.

Taarifa ya Jonathan Musau 

Share This Article