Bustani ya Uhuru Park yafunguliwa kwa umma baada ya miaka mitano

Bustani hiyo ilifunguliwa kufuatia ukarabati ambao umekuwa ukifanyika.

Dismas Otuke
1 Min Read

Baada ya kufungwa kwa jumla ya miaka mitano, hatimaye bustani ya Uhuru Park imefunguliwa kwa umma.

Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja alitangaza kufunguliwa kwa bustani hiyo jana Jumatano, baada ya kufungwa miaka mitano iliyopita na shirika lililokuwa likisimamia kaunti wakati huo la Nairobi Metropolitan.

Bustani hiyo ilifunguliwa kufuatia ukarabati ambao umekuwa ukifanyika.

Sakaja alisema bustani hiyo ilichelewa kufunguliwa kwa sababu wakandarasi walipaswa kulipwa na pia kaunti ilipaswa kukabidhiwa mradi huo baada ya kukamilika kwa ukarabati.

Raia sasa wako huru kuzuru eneo hilo la kujivinjari.

Share This Article