Nyoro ataka upinzani kutoa mwaniaji mmoja wa Urais kukabiliana na Ruto

Ingawa ametangaza azma ya kuwania Urais mwaka ujao,Nyoro amesema wataketi chini na upinzani ilia kuafikiana kuhusu mwaniaji mmoja atakayepeperusha bendera  yao .

Dismas Otuke
1 Min Read

Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro ameutaka upinzani kuwasilisha mwaniaji mmoja kukabiliana na Rais William Ruto katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Nyoro ambaye ni kiongozi wa chama cha People’s Party of Kenya, amesema njia pekee ambayo itasaidia upinzani kutwaa ushindi ni kuwa na mwaniaji mmoja.

Ingawa ametangaza azma ya kuwania Urais mwaka ujao,Nyoro amesema wataketi chini na upinzani ilia kuafikiana kuhusu mwaniaji mmoja atakayepeperusha bendera  yao .

Nyoro alikuwa akizungumza katika mkutano wa kisiasa  eneo la Subukia,kaunti ya Nakuru siku ya ya Jumamosi.

Share This Article