Chama cha wafanyakazi wa vyuo vikuu vya umma (KUSU) kimetoa ilani ya siku saba kuanza mgomo wa kitaifa endapo serikali haitatekeleza makubaliano ya nyongeza ya mwaka 2025-2029 kwa vyuo vya umma na vyuo vikuu vya umma.
Katiba Mkuu wa KUSU Dkt. Charles Mukhwaya ametangaza kuwa wataanza mgomo wa kitaifa Oktoba 2 endapo matakwa yao hayatatimizwa.
Mukhwaya ameongeza kuwa makubaliano ya awali kuhusu nyongeza ya mshahara yalisainiwa mwezi Novemba mwaka 2024 na walipaswa kusaini makubaliano mapya mwezi Februari mwaka jana lakini hilo halikutokea.
KUSU wanaishutumu serikali kwa kuwapiga chenga kila mara huku wizara ikikosa kutenga pesa za nyongeza ya mishahara.
Chama cha KUSU kinawajumuisha wafanyakazi wa vyuo vikuu na vile vya kiufundi vya umma katika idara za habari na sayansi, maafisa wa kiufundi na wafanyakazi wa maktaba.