Safari ya kufuzu kwa fainali za Kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027 itaanza rasmi leo Alhamisi kwa jumla ya mechi nane.
Katika kundi G, Brave Warriors ya Namibia watakuwa nyumbani Windhoek kuwaalika Congo Brazzavile, wakati Indomitable Lions ya Cameroon ikifungua kampeni yake nyumbani dhidi ya Comoros.
Chui wa DRC nao watamenyana na Equitorial Guinea katika kundi E, wakati Zimbabwe wakiwa wageni wa Sierra Leone.
Uganda Cranes watakuwa ziarani Tunis dhidi ya The Carthage Eagles katika kundi H, nao Botswana waitembelee Libya.
Côte d’Ivoire watakabiliana na Black Stars kutoka Ghana kundini C, kisha Mauritania watamaliza udhia na Jamhuri ya Afrika ya Kati katika kundi F.
Timu mbili bora kutoka kila kundi zitafuzu kwa fainali za 36 za AFCON.
Fainali hizo zitaandaliwa kati ya Juni 19 na Julai 17 mwakani katika mataifa ya Kenya, Tanzania na Uganda.