Rais William Ruto na mkewe Rachel, mapema leo Alhamisi wamehudhuria mechi ya mpira wa kikapu nchini Marekani kati ya klabu ya Atlanta Dream iliyomshirikisha Mkenya Madina Okot dhidi ya New York Liberty.
Okot, ambaye ni mwanafunzi wa zamani wa shule ya Kaya Tiwi, aliandikisha historia kwa kuwa Mkenya wa kwanza kuichezea ligi ya NBA kwa wanawake nchini Marekani.

Mchezaji Basketiboli huyo aliye na umri wa miaka 22, amewahi kuzichezea timu za wachezaji watatu kila upande na zile za wachezaji watano watano.
Rais Ruto yuko nchini Marekani kuhudhuria Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa mataifa (UNGA).