UNESCO kuongeza uwekezaji katika elimu, AI na mabadiliko ya tabianchi

UNESCO inapanga kuwekeza dola milioni 10  sawa na shilingi milioni 130 katika miradi kadhaa ya kimaendeleo nchini Kenya katika uvumbuzi, AI, mabadiliko ya tabianchi na elimu.

Dismas Otuke
1 Min Read

Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), limekubali kuongeza uwekezaji wake katika sekta za elimu, uvumbuzi, mabadiliko ya tabianchi, akili unde, AI na ukuzaji maarifa nchini Kenya.

Haya yalijiri baada ya Rais William Ruto kukutana na Mkurugenzi wa UNESCO Khaled El-Enanywa, pembezoni mwa Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) jijini New York nchini Marekani.

UNESCO inapanga kuwekeza dola milioni 10  sawa na shilingi milioni 130 katika miradi kadhaa ya kimaendeleo nchini Kenya katika uvumbuzi, AI, mabadiliko ya tabianchi na elimu.

Mazungumzo hayo pia yalijikita katika ushirikiano kwa makala ya mwaka ujao ya kipute cha Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) na Mashindano ya Riadha Duniani mwaka 2029, na ukuzaji wa elimu, tamaduni, sayansi na michezo kama chambo cha kubuni fursa za ajira.

Kenya itaandaa kongamano la UNESCO  duniani Januari mwaka ujao kuhusu elimu kwa maendeleo endelevu.

Share This Article