Chipukizi wa Kenya kumenyana na Tanzania kufuzu AFCON chini ya miaka 17

Kundi A linajumuisha wenyeji Rwanda,Sudan,Somalia na Sudan Kusini huku Uganda,Ethiopia na Burundi zikirushwa kundi B

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya kwa wanaume wasiozidi umri wa miaka 17 imepangwa kundi moja la C, pamoja  na majirani Tanzania na Djibouti  katika mechi za ukanda wa CECAFA kufuzu kwa Kombe la AFCON mwaka ujao.

Mechi hizo zitaandaliwa mjini Kigali Rwanda kati ya Oktoba 10 na 19 mwaka huu.

Kundi A linajumuisha wenyeji Rwanda,Sudan,Somalia na Sudan Kusini huku Uganda,Ethiopia na Burundi zikirushwa kundi B.

Timu bora kutoka kila kundi itafuzu kwa nusu fainali pamoja na timu ya pili bora kutoka makundi yote matatu.

Share This Article