Nigeria kukabana koo na Japan,fainali ya Kombe la Dunia mabanati chini ya miaka 17

Fainali hiyo itatanguliwa na mechi ya kuwania nishani ya shaba baina ya Brazil na mabingwa watetezi  Korea Kaskazini.

Dismas Otuke
1 Min Read

The Flamingoes ya Nigeria watashuka katika uwanja wa Mohammed VI nchini Morocco,  dhidi ya Japan,katika fainali ya Kombe la Dunia kwa  wasichana chini ya umri wa miaka 17.

Fainali hiyo itatanguliwa na mechi ya kuwania nishani ya shaba baina ya Brazil na mabingwa watetezi  Korea Kaskazini.

Nigeria watamenyana na Japan kuanzia saa tatu unusu,waakilishi wa Afrika wakiwinda taji ya kwanza nao Japan wakiwania kombe la pili.

Nigeria walifuzu kwa fainali baada ya kuwadhalilisha  Brazil  mabao 4-1 nao Japan wakawabwaga Korea Kaskazini mgoli 4-1 kufuatia sare ya 1-1.

 

Share This Article