Starlets waimarisha mazoezi kujiandaa kwa Kombe la Dunia

Kipute cha Kombe la Dunia kitaandaliwa nchini Morocco kati ya Oktoba  17 na Novemba 17.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya kwa wasichana chini ya umri wa miaka 17,Junior  Starlets imeendeleza mazoezi yake kujiandaa kushiriki fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya pili .

Starlets wanaofunzwa na kocha Midlred Cheche, wataondoa nchini Ijumaa wiki hii kwenda Uhispania, ambapo watacheza mechi kadhaa za kujinoa makali.

Kenya itafungua Kombe la Dunia dhidi ya Uchina tarehe 19 mwezi ujao katika kundi E,kabla ya kupimana nguvu na Marekani Oktoba 22, na kuhitimisha ratiba dhidi ya Samoa siku tatu baadaye.

Kipute cha Kombe la Dunia kitaandaliwa nchini Morocco kati ya Oktoba  17 na Novemba 17.

Share This Article