Kenya ilinyakua ubingwa wa jumla katika makala ya mwaka huu ya mashindano ya mbio za barabara duniani zilizokamilika Jumapili mjini Copenhagen,Denmark.
Kenya ilizoa jumla ya nishani 7 ,dhahabu 3,fedha 3 na shaba moja.
Agnes Jebet Ngetich alishinda nishani ya dhahabu katika mbio za nusu marathoni huku pia timu ya wanawake ya kilomita 21 na ile ya wanaume zikinyakua dhahabu kila moja.
Ethiopia ilimaliza ya pili kwa dhahabu 1 fedha 2 na shaba 1, wakati Eritrea ikiridhia dhahabu 1 na shaba 1,huku Ufaransa,Uswidi na Ujerumani zikitwaa dhahabu moja kila moja.