Marekani yalenga kufuzu raundi ya 32 bora

Marekani wana alama tatu sawia na Australia katika kundi D katika kipute kinachoendelea cha Kombe la Dunia.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wenyeji wenza wa Kombe la Dunia, Marekani, watalenga kujikatia tiketi kwa raundi ya 32 bora watakaporejea uwanjani kwa mchuano wa kundi D Ijumaa usiku dhidi ya Australia.

Marekani waliosajili ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi Paraguay katika mechi ya ufunguzi, watashuka uwanjani Seattle dhidi ya Socceroos wakifahamu kuwa ushindi utawawezesha kuongoza kundi hilo.

Marekani wana alama tatu sawia na Australia katika kundi D.

Uturuki watavaana na Paraguay katika mechi nyingine mapema Jumamosi.

Katika mechi za kundi C, Atlas Lions ya Morocco watamenyana na Scotland saa saba usiku, kabla ya mabingwa mara tano Brazil kupimana ubabe na Haiti saa tisa unusu alfajiri.

Scotland wanaongoza kundi hilo kwa pointi 3, wakifuatwa na Barzil na Morocco kwa alama moja kila moja.

Share This Article