Wenyeji pekee wa Kombe la Dunia waliosalia Marekani watapimana nguvu na Ubelgiji Jumanne saa tisa alfajiri uwanjani Dallas.
Marekani inayonolewa makali na Mauricio Pochettino, itakuwa ikichuana na Ubelgiji kwa mara ya pili tangu Ubelgiji iwashinde Marekani katika muda wa ziada kwenye Kombe la Dunia mwaka 2014.
Ushindi pekee wa Marekani dhidi ya Ubelgiji ulikuwa wa 3-0 katika Kombe la Dunia mwaka 1930, na baadaye kupoteza mechi sita zilizofuatia.
Marekani iliongoza kundi D kwa alama 6, wakishinda mechi mbili dhidi ya Australia na Paraguay kabla ya kupigwa na Uturuki na hatimaye kuwatema nje Bosnia Herzegovina 2-0 katika hatua ya 32.

The Red Devils ya Ubelgiji iliongoza kundi G ikitoka sare na Misri na Iran na kuishinda New Zealand kabla ya kutoka nyuma na kuwatema nje Senegal 3- katika raundi ya 32.
Mshindi wa mechi hiyo atakutana na mshindi kati ya Ureno na Uhispania katika robo fainali.