Timu ya taifa Kenya kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 imebanduliwa nje ya michuano ya kufuzu kwa mashindano ya bara Afrika FACON mwaka ujao baada ya kutoka sare ya bao moja na Sudan Kusini katika mchuano wa mwisho Jumamosi adhuhuri katika uwanja wa Uhuru ,jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Kenya wanaofunzwa na kocha Gilbert Selebwa walihitaji ushindi ili kufuzu kwa nusu fainali lakini sare hiyo ikawatupa nje ya safari ya kuelekea Ghana kwa fainali za AFCON mwaka ujao.
Mabingwa wa michuano hiyo ya CECAFA watafuzu kushiriki fainali za AFCON mwaka ujao nchini Ghana.