Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP), imefanikisha hukumu ya miaka 25 dhidi ya mwanamume analiyeshtakiwa kwa kumdhulumu kimapenzi mtoto wa umri wa miaka 15 aliye na matatizo ya akili.
Mwanamume huyo alishtakiwa kuambatana na sheria ya dhuluma za kimapenzi sehemu ya 8(1) pamoja na sehemu ya 8(3).
Upande wa mashtaka ukiongozwa na Justice Mugambi, uliwasilisha ushahdi wa kutosha kutoka kwa mlalamishi na mashahidi wengine watano, pamoja na ripoti za matibabu, huku mahakama ikithibitisha kuwa shahidi hizo zilikuwa za kuaminika na hivyo kutoa kifungo hicho.
Kupitia ukurasa wa X, afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, ilisema hukumu hiyo n shara ya kujitolea kwake kuhakikisha haki inapatikana kwa waathiriwa, hususan wale wanaowadhulumu watoto kimapenzi.
Hata hivyo, mwanamume huyo amepewa siku 14 kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.