Rais William Ruto ameipongeza timu ya taifa ya Kenya ya mpira wa wavu kwa wanawake Malkia Strikers, baada ya kuipiku Cameroon siku ya Alhamisi na kufuzu kwa fainali.
Rasi kupitia kwa kurasa zake za mitandao ya kijamii alisema anafaharikia matokeo ya Malkia Strikers huku akiwatakia kila heri katika mchezo wa fainali Ijumaa usiku uwanjani Kasarani dhidi ya Misri.
Kenya wanawinda kombe la 11 na tiketi ya kufuzu kwa mashindano ya Dunia mwakani.
Malkia watarejea uwanjani Ijumaa usiku kwa mechi ya fainali wakijivunia kutopoteza mechi hadi sasa huku wakishindwa seti moja peke.