Shirika la Kukadiria Ubora wa Bidhaa nchini (KEBS) limeandaa sheria kadhaa mpya zinazolenga kuimarisha uangalizi wa soko, uthibitishaji wa bidhaa na kulinda watumiaji.
Shirika hilo liko mbioni kuziba mianya inayotumiwa katika uagizaji usiodhibitiwa wa bidhaa kutokana na maendeleo ya kasi ya teknolojia na mabadiliko ya utendaji kazi.
Sheria zilizopendekezwa zinajumuisha Sheria zya Viwango vya (Uthibitishaji wa Bidhaa) 2026, Sheria ya Viwango vya (Uangalizi wa Masoko) 2026 na Sheria ya Viwango vya (Kisayansi na Metrolojia ya Viwanda) 2026 miongoni mwa zingine.
Kulingana na KEBS, baadhi ya sheria za sasa zimekuwepo kwa zaidi ya miongo minne, huku sheria ya uthibitishaji wa bidhaa ikianzishwa mwaka 1977 na hivyo kukosa kutilia maanani mabadiliko ya sasa katika sekta hiyo.