Sheria mpya ya kuingia na kuondoka nchini China inaanza kutekelezwa leo Jumatano wakati serikali ikisema inalenga kulinda uhuru wa kitaifa, usalama na maslahi ya maendeleo ya nchi hiyo.
Sheria hiyo inawezesha mamlaka za China kupiga marufuku raia wake wanaokiuka sheria za uagizaji na usafirishaji nje wa teknolojia kuondoka nchini humo.
Katika kuchukua hatua hiyo, serikali inasema uhamishaji unaokiuka sheria wa teknolojia nje ya nchi umeathiri mno usalama wa viwanda na teknolojia.
Inaonekana China inalenga kuzuia teknolojia ya kisasa kusafirishwa nje ya nchi kwa kuweka vikwazo vya usafiri kwa wabobezi wa masuala ya teknolojia.
Sheria hiyo inawataka watu wanaoingia au kuondoka nchini China kushirikiana na mamlaka wanapotakiwa kuwasilisha au kutoa waraka au data ya kielektroniki ili kwa minajili ya kuthibitishwa.