Kenya kubaini hatima ya kuandaa mashindano ya Riadha Duniani 2029 Jumanne

Awali Kenya ilipewa jukumu la kuandaa mashindano ya Dunia kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 18 mwaka 2017, na yale chini ya chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 mwaka 2021,na mashindano ya Dunia ya mbio za nyika mwaka 2007.

Dismas Otuke
1 Min Read

Hatima ya Kenya kuandaa mashindano ya Riadha Duniani mwaka 2029 au mwaka 2031 itabainika Jumanne ,Septemba 15 ,wakati baraza kuu la Shirikisho la Riadha Ulimwenguni litakapotoa tangazo rasmi.

Jiji la Nairobi linawania maandalizi ya mojawapo wa mashindano ya ya Dunia ya mwaka 2029 au 2031, ingawa upinzani mkali unatarajiwa kutoka kwa miji ya Rome-Italia,Munich-Ujerumani na London-Uingereza.

Kenya inawania maandalizi hayo baada ya kupoteza makala ya mwaka ujao kwa Beijing-Uchina.

Aidha,Kenya inalenga kuwa taifa la kwanza Afrika kutwikwa jukumu la kuandaa mashindano hayo ya kila baada ya miaka miwili.

Awali Kenya ilipewa jukumu la kuandaa mashindano ya Dunia kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 18 mwaka 2017, na yale chini ya chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 mwaka 2021,na mashindano ya Dunia ya mbio za nyika mwaka 2007.

Share This Article