Rising Stars yawasili Tanzania kusaka tiketi ya AFCON

Kenya itafungua kampeini ya kufuzu kundini C, dhidi ya Burundi Septemba 17,kabla ya kumenyana  na Sudan Kusini.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya ya soka kwa chipukizi walio chini ya umri wa miaka 20,Rising Stars ,imewasili Tanzania mapema Jumatatu kushiriki mashindano ya ukanda wa CECAFA, kufuzu kwa fainali za Kombe la mataifa ya Afrika (AFCON).

Kenya itafungua kampeini ya kufuzu kundini C, dhidi ya Burundi Septemba 17,kabla ya kumenyana  na Sudan Kusini siku mbili baadaye,mechi zote zikipigwa katika uwanja wa Uhuru,jijini Dar es Salaam-Tanzania.

Jumla ya mataifa  tisa yaliyotengwa katika makundi matatu ya timu tatu tatu yanashiriki mashindano hayo huku timu mbili bora kifuzu kwa mashindano ya AFCON mwaka ujao nchini Ghana.

Kundi A  linajumuisha wenyeji Tanzania,Ethiopia na Rwanda nalo kundi B, likisheheni Uganda na Eritrea.

Wenyeji Tanzania wanatetea taji hiyo baada ya kuwashinda Kenya mabao 2-1, kwenye fainali ya mwaka 2024.

Fainali za AFCON kwa mabarubaru zitaandaliwa  mwaka ujao nchini Ghana.

 

 

 

Share This Article