Timu ya taifa ya Kenya,Malkia Strikers itashuka uwanjani Kasarani Jumamosi jioni kwa mechi ya raundi ya 16 dhidi ya Nigeria katika mashindano ya kuwania Kombe la mataifa ya Afrika.
Malkia Strikers ambao walishinda mechi zao mbili za kundi A watalenga ushindi ili kufuzu kwa robo fainali huku wakijizatiti kutetea ubingwa wao na kufuzu kwa mashindano ya Dunia mwaka ujao.
Katika mechi nyingine za raundi ya 16 siku ya Jumamosi,Uganda watakabiliana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuanzia saa saba ,kabla ya Algeria kumenyana na Senegal saa kumi kisha Kenya wafunge ratiba saa moja usiku.
Mechi zaidi zitachezwa Jumapili huku fainali yake ikipigwa Septemba 5.