Shirikisho la soka nchini Senegal (FSF)limemteua nyota wa zamani wa Ufaransa Patrick Vieira kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Teranga Lions.
Vieira anatwaa mikoba ya ukufunzi wa Senegal kutoka kwa Pape Thiaw,aliyepigwa kumbo na benchi yote ya kiufundi kufuatia matokeo mabovu katika Kombe la Dunia mwezi jana.
Senegal ilibanduliwa nje ya kipute cha Kombe la dunia na Ubelgiji katika raundi ya 16 .
Kibarua kikubwa kinachomsubiri Vieira ambaye ni nguli wa zamani wa Arsenal, ni kuandaa Teranga Lions kwa mechi za kufuzu Kombe la AFCON mwaka ujao.