Safari za ndege Garissa zaongezeka baada ya uwanja kukarabatiwa

Martin Mwanje
1 Min Read

Mwezi mmoja baada ya shughuli kurejelewa katika Uwanja wa Ndege wa Garissa, mashirika ya ndege yameanzisha safari za ndege kwenye njia ya kati ya Nairobi na Garissa. 

Uwanja huo ulikarabatiwa kwa kitita cha shilingi milioni 710 kwa pamoja na serikali kuu na ile ya kaunti ya Garissa.

Ni ukarabati unaoonekana kufungua milango ya fursa mpya kwa wakazi wa Garissa na eneo hilo kwa upana.

Jana Jumatano, Shirika la Ndege la Skyward Airlines lilizindua safari yake ya kwanza ya ndege kupitia njia hiyo.

Ndege hiyo ikitarajiwa kufanya safari nne kwenye njia hiyo siku za Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumapili huku kila safari ikighaarimu shilingi 9,000.

Gavana wa Garissa Nathif Jama amesifia hatua hiyo akisema itaboresha safari za kwenda eneo la Garissa, kuwezesha usafirishaji wa bidhaa na usafiri wa watu, na kuchangia ukuaji wa utalii, biashara, uwekezaji na shughuli za kijamii na kiuchumi.

 

Share This Article