Waziri Kagwe atoa hakikisho la utoshelevu wa chakula

Martin Mwanje
1 Min Read

Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe amewahakikishia Wakenya kuwa nchi hii itasalia kuwa na chakula cha kutosha licha ya athari za kiangazi na hali za hewa zisizotabirika. 

Akizungumza katika kaunti ya Trans Nzoia, alikokadiria athari za kiangazi kwa uzalishaji wa mahindi, Kagwe alisema serikali inatarajia uzalishaji wa zao hilo kupungua kwa sababu ya kiangazi.

Hata hivyo, amesema serikali imeweka mikakati ya kuikinga nchi dhidi ya uhaba wa chakula.

Kulingana naye, Kenya itaagiza mahindi kupiga jeki uzalishaji wa ndani ya nchi, huku serikali ikitarajia kuagiza mahindi zaidi kutoka eneo la COMESA.

Waziri amesema serikali pia pia imeridhishwa na akiba ya mbegu za mahindi licha ya kiangazi kinachoshuhudiwa.

Alikadiria kuwa kati ya asilimia 25 na 30 percent ya mbegu hizo inaweza ikapotea, lakini ameongeza kuwa nchi hii bado ina mbegu za kutoshja kuwasaidia wakulima wakati wa msimu ujao wa upanzi.

Kagwe ameashiria hali zinazobadilika za hali ya hewa zinailazimu serikali kuwazia tena mbinu zake kwa uzalishaji wa kilimo na mifugo.

Share This Article