Ni kwa nini nchi za Afrika na Amerika Kusini zinamuunga mkono Infantino

Dismas Otuke
2 Min Read

Rais wa FIFA Gianni Infantino anapitia mwezi mgumu wa kipindi cha mwongo mmoja ambao amekuwa afisini.

Mpango wake uliotibuka wa kuuza hisa za Kombe la Dunia kwa waekezaji wa kibinafsi zimeibua hisia za ukosefu wa uaminifu wa FIFA kutoka kwa mashirikisho ya ulaya UEFA,bara Asia(AFC),na eneo la marekani kaskazini na CONCACAF.

Shirikisho la soka nchini linamtaka Infantinho ajiuzulu huku Uingereza ikiondoa uungaji mkono kuchaguliwa tena .

Mawakili wa UEFA wanatafakari kumshtaki Infantinho .

Mataifa ya Africa na Amerika Kusini yanaonekana kumuunga mkono Infanthino .

Mataifa 54 ya Afrika ambayo ni zaidi ya robo ya wanachama wote yametangaza azma ya kusimama na Infantino tangu mapema mwezi Agosti .

Shirikisho la soka nchini Argentina limetangaza kumuunga mkono Infantinho huku Mexico, ikikaidi msimamo wa CACNCAF na kusima kidete naye wakati Rais wa Marekani Donald Trump, akionya kuwa kubanduliwa kwa Infantino huenda kukawa na Athari kubwa.

Licha ya mataifa ya Ulaya kutaka kinara huyo atimuliwe aidha, yanapaswa kuangalia mchngo wake na ufanisi tangu atwae mamlaka mwaka 2016kuoka kwa Sepp Blatter mwaka 2016.

Katika kipimndi chake afisini idadi ya timu zinazoshiriki Kombe la Dunia zimeongezeka kutoka 32 hadi 48.

Katika kipindi chake cha utawala FIFA imeongeza uwekezaji wake katika mabara ya Afrika,Asia na CONCACAF .

Aidha, mashindano nje ya ulaya kama vile Kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) yameongeza pesa yanyiokusanya kuoitia kwa uuuzaji haki za kutangaza mashindano badala ya kutegemea FIFA kila mara.

Sio busara kwa maswali yote yaliyoibuliwa na UEFA kuhusu mpango wa FIFA kuuza hisa ambao umgetoa fursa kwa waekezaji kibinafsi.

Share This Article