Morocco imeteuliwa kuandaa kongamano la 77 la shirikisho la soka ulimwenguni (FIFA), ambalo litakuwa la uchaguzi wa mrithi wa Rais Gianni Infantino.
Uteuzi wa Morocco kuwa mwenyeji wa uchaguzi huo unatokana na hatua kubwa zilizoafikiwa na taifa hilo la kaskazini mwa Afrika.
Atlas Lions ni ya kwanza Afrika katika msimamo wa dunia (FIFA ) ikiwa ya nane kwa jumla, na pia ilicheza hadi nusu fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar.

Pia Morocco ilitwikwa jukumu la kuandaa fainali za Kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2025, na itakuwa mwenyeji mwenza wa Kombe la Dunia mwaka 2030, pamoja na majirani Uhispania na Ureno.
Itakuwa mara ya pili kwa uchaguzi wa FIFA kufanyika Afrika,baada ya mji wa Kigali nchini Rwanda, kuandaa kongamano la mwaka 2023 ambapo Infantino alichaguliwa kwa muhula wa pili.