Katibu wa Madini Harry Kimtai, ametoa wito wa jamii kushirikishwa kikamilifu katika uhifadhi wa misitu.
Kulingana na Kimataifa, usimamizi endelevu wa misitu ni sharti uhusishwe na kuimarika kwa maisha ya wananchi.
Akizungumza katika msitu wa Saboti, eneo la Mlima Elgon wakati wa mkutano na wanachama wa kuhifadhi msitu, Kimtai alitoa changamoto kwa jamii kutumia vyema fursa zilizopo kwa kuhakikisha usimamizi endelevu wa misitu na shughuli za kilimo.
“Uhifadhi wa misitu na kuwezesha jamii unaambatana na kuwezesha jamii na kuhakikisha mazingira bora na mustakabali wenye ufanisi,” alisema Kimtai.
Aidha, Kimtai aliangazia jukumu muhimu jamii zinapaswa kutekeleza ili kuimarisha utoshelevu wa chakula.
Matamshi yake yanajiri baada ya aguzo la Waziri wa Mazingira, Mabadiliko ya Tabianchi na Misitu kwa Huduma ya Taifa ya Misitu kuimarisha ushirikiano na vyama vya jamii vya uhufadhi wa misitu.
Mpango huo unalenga kupanua upanzi wa misitu, kuimarisha ushiriki wa jamii na kuboresha maisha.