Kenya ilinyakua nishani tatu jana ;dhahabu,fedha na shaba katika siku ya kwanza ya mashindano ya Riadha duniani kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20 mjini Oregon,Marekani.
Frankline Kibet alishinda medali ya dhahabu ya mita 5,000 abaada ya kutimka mbio hizo kwa muda wa dakika 13 sekunde 28.27, huku nahodha Nehemia Kipngeno akinyakua fedha kwa dakika 13 sekunde 30.09.
Nishani ya shaba ilitwaliwa na Demetew Kebede wa Ethiopia.
Awali Nahodha mwenza wa Kenya Joyline Chepkemoi, alikuwa ameshinda shaba ya fainali ya mita 5000 kwa kutumia dakika 15 sekunde 9.8,akifuatwa na Cynthia Chepkurui, katika nafasi ya nne.
Charity Cherop wa Uganda alitwaa dhahabu huku fedha ikimwendea Shito Gumi kutoka EWthiopia.
Kenya ni ya kwanza katika jedwali la nishani baada ya siku ya kwanza kwa dhahabu 1,fedha 1 na shaba 1,ikifuatwa na Marekani ,Brazil na Uganda kwa dhahabu moja kila moja.