Seneti: Mishahara katika serikali za kaunti kikwazo kwa maendeleo

Ripoti hiyo ilionyesha fedha zilizotengewa maendeleo zilipungua, huku kaunti nyingi zikikosa kuzingatia hitaji la kutumia asilimia 30 pekee ya fedha zake kwa miradi ya maendeleo.

Tom Mathinji
2 Min Read
Bunge la Senate.

Bunge la Seneti limefichua kuwa ongezeko la mishahara na marupurupu yasiyostahili katika serikali za kaunti,  zinawanyima wakenya maendeleo na huduma katika kaunti zote 47.

Ripoti ya Bunge la Seneti kuhusu ukadiriaji wa matumizi ya fedha,  imefichua kwamba kaunti za Nairobi, Bomet, Busia, Kakamega na Kisumu, ni miongoni mwa kaunti ambazo hazijatumia ipasavyo rasilimali za umma huku kaunti zilizowajibikia vyema rasilimali za umma zikiwa ni pamoja na Embu, Narok, Wajir, Kitui na Kilifi, miongoni mwa nyingine.

Kulingana na ripoti  hiyo, Magavana na Wanachama wa Mabunge ya Kaunti, wamepatia kipaumbele nyongeza ya mishahara na marupurupu, pamoja na shughuli nyingine, bila kuwajali walipa ushuru.

Ripoti hiyo ilionyesha fedha zilizotengewa maendeleo zilipungua, huku kaunti nyingi zikikosa kuzingatia hitaji la kutumia asilimia 30 pekee ya fedha zake kwa miradi ya maendeleo

Miongoni mwa kaunti zilizokosa kuwajibikia matumizi ya rasilimali za umma ni Nairobi, Bomet, Busia, Kakamega na Kisumu, huku kaunti za Embu, Narok, Wajir, Kitui na Kilifi zikiorodheshwa miongoni mwa kaunti zilizowajibika

Gavana wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja, Gavana wa Nyamira Amos Nyaribo na mwenzake wa Kajiado Joseph Ole Lenku walikosolewa kwa kupatia kipaumbele mishahara na marupurupu kupita kiwango cha asilimia 35, ilhali wenzao kutoka kaunti za Embu, Nakuru, Narok na Kilifi waliwajibika katika usimamizi wa mishahara na marupurupu mtawalia.

Share This Article