Mashindano ya shule za Upili: Kakamega, Soweto, Joga na Chesamisi zafuzu fainali

KBC Digital News
1 Min Read
Shule ya Upili ya wavulana ya Kakamega yafuzu kwa fainali ya mchezo wa soka kwenye mashindano ya shule za upili yanayoendelea Thika.

Shule za wavulana za Kakamega na Yala leo Jumatano zimetinga katika fainali ya kesho Alhamisi ya mashindano ya kitaifa baina ya shule za upili (KSSSA) yanayoendelea mjini Thika.

Kakamega ilifuzu baada ya kuifunga shule ya upili ya Menengai 2-1, huku shule ya upili ya Yala ikifuzu baada ya kuifunga shule ya upili ya Takaba 2-0.

Nao warembo wa St. Joseph Kitale na Nyakach pia walijikatia tiketi hizo kwa kuwalemea Archbishop Njenga na Raila Odinga Centre bao moja kwa nunge na mabao manne kwa bila mtawalia.

Kwenye voliboli ya wavulana, Chesamisi na Chepsaita watakwaruzana baada ya kuwalaza Masara na Matiliku seti tatu bila jibu na seti tatu kwa yai mtawalia.

Kwa upande mwingine, vipusa wa Chesogon na Soweto watakabana koo kufuatia ushindi wa seti tatu kwa sufuri na tatu kwa moja dhidi ya Kwanzanze na Mwitoti mtawalia.

Zaidi ya fainali, timu hizo pia zitawakilisha nchi katika mashindano ya Afrika Mashariki baina ya shule za upili  mjini Morogoro nchini Tanzania baadaye mwezi huu.

Share This Article