Watu 14 wafariki kwenye maporomoko ya ardhi Ethiopia

Kulingana na mamlaka nchini humo, watu kadhaa hawajulikani waliko baada ya ajali hiyo iliyotokea siku ya Jumatatu, huku shughuli za uokoaji zikiendelea.

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu 14 wafariki kwenye maporomoko ya ardhi Ethiopia.

Watu 14 wamefariki na wengine saba kujeruhiwa kwenye maporomoko ya ardhi katika eneo la Amhara nchini Ethiopia.

Kulingana na mamlaka nchini humo, watu kadhaa hawajulikani waliko baada ya ajali hiyo iliyotokea siku ya Jumatatu, huku shughuli za uokoaji zikiendelea.

Maporomoko hayo yalitokea wakati mamia ya waumini walikusanyika kwa ibada ya utakaso, ambayo ni maarufu kwa wanaotafuta uponyaji wa magonjwa sugu.

Meneja wa dayosisi ya St. Mary Monastery ambako maporomoko hayo yalitokea Megabe Hadis Neka Tibeb Ababu, alisema ajali hiyo ilitokea saa moja asubuhi saa za taifa hilo, na wengi waliofariki walikusanyika kupokea maji matakatifu.

Kulingana na meneja huyo, watu kadhaa wanaaminika wamenaswa kwenye vifusi.

“Watu 11 waliofariki walizikwa katika eneo hilo la St. Mary Monastery, huku miili ya waliosalia ikitumwa makwao,” aliongeza Meneja huyo akisema baadhi ya miili haikuweza kutambuliwa.

Kundi la wataalam limepelekwa kusaidia katika shughuli za uokoaji, kulingana na taarifa ya utawala wa sehemu hiyo.

Share This Article